
Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, hali ya kisiasa bado ni tete huko Kinshasa, ambapo kukamatwa kwa watu walio karibu na rais wa zamani Joseph Kabila kunaendelea. Siku ya Jumamosi usiku, watu wenye silaha nzito kutoka kwa kikosi cha usalama wa rais wa Kongo walimkamata Aubin Minaku, Spika wa zamani wa Bunge la taifa na naibu kiongozi wa chama cha PPRD, chama tawala cha zamani, ambacho kinalaani kile kinachokiita “utekaji nyara.”
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Kukamatwa kwa Aubin Minaku kumekasirisha chama cha Kabila, haswa kwani Emmanuel Ramazani Shadary, katibu wa kudumu wa chama hicho, anashikiliwa na idara hiyo ya usalama wa rais.
Ferdinand Kambere, naibu katibu mkuu wa PPRD, chama cha Joseph Kabila, amewasiliana na Pascal Mulegwa, mwandishi wetu huko Kinshasa.
“Naibu kiongozi wa chama Aubin Minaku alikuwa mwathirika wa utekaji nyara uliopangwa na wale walio madarakani. Chama bado hakijui aliko. PPRD inalaani mbinu hizi zilizopitwa na wakati! Imekuwa mwezi mmoja tangu mwenzetu, katibu mkuu (Emmanuel Ramazani Shadary), kutekwa nyara, na hadi leo, mawakili wake hawajaruhusiwa kuwasiliana naye.
Tunalaani vitendo hivi vilivyopitwa, kumhusisha uhalifu mtu kwa sababu yuko katika upinzani au kutokana na msimamo wa upinzani kuhusu hali inayojiri nchini.
Leo, tunaomba kuachiliwa mara moja na bila masharti kwa wenzi wetu waliokamatwa na wengine kadhaa ambao wamekamatwa katika mazingia kama haya, kwa lengo la kuwanyamazisha wapinzani.”
Kulingana na Ferdinand Kambere, hili ni jaribio la kuanzisha aina ya “udikteta au udhalimu” nchini DRC.