Shirika la ujasusi la Iran limetangaza kuwa limemkamata mmoja wa maajenti wa ngazi ya juu aliyepewa mafunzo na mashirika ya ujasusi ya Marekani na Israel.
Shirika la upelelezi la Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) limefanikiwa jumtia nguvuni kinara wa magaidi wa uutawala wa Kizayuni na Marekani baada ya miezi kadhaa ya kumfuatilia kimyakimya.
Mtu aliyekamatwa anajulikana kwa jina Nazanin Baradaran ambaye ana vitambulisho kadhaa vya bandia na alikuwa akiongoza mradi wa siri wa mapinduzi laini na kuunda mtandao wa hujuma za mtandaoni dhidi ya Iran.
Nazanin aliyekuwa akifanya kazi zake chini ya mwavuli wa kuwa makamu wa rais wa taasisi ya kifikra, alikuwa akiandaa mpango wa hatua kwa hatua wa kuyumbisha amani na usalama wa Iran.
Mpango huu, ambao ulitayarishwa mwaka 2022, ulipaswa kutekelezwa mwaka 2025-2026 na kuwasilishwa Umoja wa Mataifa kwa ajili ya kutambuliwa serikali ya upinzani ya Iran.
Vilevile walijaribu kuharibu sura ya Jamhuri ya Kiislamu kwa kuunda jeshi la mtandao.
Kwa mujibu wa shirika la ujasusi la Iran, timu kadhaa za usalama zilifuatilia mawasiliano ya kigeni ya Nazanin Baradaran ambaye anatambulika katika mtandao wa mawakala wa Marekani na Israel kama Raha Parham, na kurikodi mienendo yake ya uwanjani, na vilevile mtandao aliokuwa akiufanyia kazi, na hatimaye kukamatwa baada ya kukamilishwa operesheni ya upelelezi.

Raha Parham, ambaye alikuwa na jukumu la kusimamia mtandao wa ndani ya Iran wa vibaraka wa Marekani na Israel, aliwasilisha mpango sawa na ule uliotekelezwa Syria kwa ajili ya Iran katika mkutano wake na Tom Cotton, seneta mpenda vita wa Marekani.