Norlan Yerkembayev Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai (SCO) amelaani vikali hujuma za kigaidi na uharibifu wa hivi karibuni katika mji wa Tehran na miji mingine ya Iran iliyoathiriwa wakati wa maandamano ya amani ya wananchi.

Yerkembayev jana alibainisha masikitiko yake makubwa na akatoa mkono wa pole kwa serikali, wananchi wa Iran na familia za wahanga wa vghasia na machafuko yakaribuni, na kuwatakia ahueni ya haraka majeruhi.

Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai amezungumza kwa simu na Waziri wa Mambo ya Nje Abbas Araghchi na kujadili matukio ya kikanda na kimataifa. Aidha amesisitiza umuhimu wa mshikamano na kushirikiano mataiga ya jumuiya hiyo ili kutatua tatizo la ugaidi na uingiliaji wa nchi ajinabi. 

Katika mazungumzo hayo ya simu, Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran ameashiria matukio ya karibuni nchini na kuelezea namna maandamano ya amani ya wananchi yalivyoporwa na magaidi mamluki waliopewa mafunzo. 

Sayyid Abbas Aragchi amesisitiza kuwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran itahami na kulinda mamlaka yake ya kitaifa,  na usalama wa raia mkabala wa ugaidi unaoungwamkono na utawala wa Kizayuni na Marekani.

Aragchi pia amempongeza msimamo wa Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai wa kulaani ugaidi na uingiliaji wa nchi ajinabi katika masuala ya ndani ya Iran. Aragchi pia amesisitiza wajibu wa pamoja wa nchi zote kushirikiana ili kuzuia na kukabiliana na ugaidi.

Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai aidha ametilia mkazo kuhusu msimamo wa pamoja wa nchi wanachama wa jumuiya hiyo na kutaka kuheshimiwa mamlaka ya kujitawala nchi, uhuru, umoja wa ardhi nzima,  manufaa ya pande zote, na kutoingilia mambo ya ndani ya nchi nyingine.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *