Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Ndugu Kenani Laban Kihongosi, amemuagiza Waziri wa Afya Mhe. Mohamedy Mchengerwa kuhakikisha gari la wagonjwa (Ambulance) linafika katika Hospitali ya Wilaya Singida Vijijini haraka iwezekanavyo.

Alitoa rai hiyo leo Jumatatu January 19 baada ya kukagua ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Singida Vijijini, iliyopo Ilongero, mradi unaogharimu Tsh. bilioni 3.7 katika siku ya pili ya ziara yake ya siku tano mkoani Singida.

MNEC Kihongosi alimpigia simu Waziri wa Afya Mhe. Mohamedy Mchengerwa na kuagiza wizara hiyo kuhakikisha gari hilo linafika kwa wakati.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *