
Hii inaashiria sura mpya katika jaribio la mapinduzi nchini Burkina Faso mnamo Januari 3. Luteni Kanali Paul-Henri Sandaogo Damiba amekamatwa na kufukuzwa kutoka Lome, nchini Togo, ambapo alikuwa akiishi uhamishoni tangu mwezi Oktoba 2022. Kanali Damiba ambaye alikuwa akiishi uhamishoni nchini Togo baada ya kupinduliwa na Kapteni Ibrahim Traoré, anatuhumiwa mara kwa mara na Lome kwa kujaribu kuvuruga utawala wa kijeshi uliomtimuwa mamlakani.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Kulingana na chanzo kilicho karibu na afisa huyo wa kijeshi, Luteni Kanali Damiba alichukuliwa kutoka nyumbani kwake katika kitongoji cha “Lomé 2” hadi Mahakama ya Rufaa siku ya Ijumaa, Januari 16. Mahakamani, jaji alitoa uamuzi kuhusu hatima yake na kukubali ombi la kurejeshwa nyumbani kutoka kwa mamlaka ya Burkina Faso.
Mara tu uamuzi ulipotolewa, baadhi ya mali zake binafsi zililetwa kwake kutoka kwenye jengo la “Six villas” ambapo alikuwa akiishi. “Six villas,” ni eneo lenye ulinzi mkali wa mji mkuu wa Togo, ambapo Paul-Henri Damiba hakuwa huru kabisa kutembea apendavyo.
Wanajeshi waliokuwa wakimsindikiza walimpeleka uwanja wa ndege siku ya Jumamosi, Januari 17, na kumsafirisha kwenda nchi ambayo bado haijathibitishwa.
Hatua hii ilichukuliwa kulinagana na nadharia ya Ouagadougou ya jaribio la njama dhidi ya utawala wa Ibrahim Traoré. Rais huyo wa zamani wa Burkina Faso, anashutumiwa mara kwa mara na jeshi la sasa kwa kutaka kufanya mapinduzi. Mpango wa hivi karibuni unaodaiwa ulishindwa, kulingana na Ouagadougou, mnamo Januari 3.
Kwa wakati huu, mamlaka huko Ouagadougou wala ile ya Lome hawajatoa maoni kuhusu hatua hii ya kurejeshwa nyumbani kwa rais huyu wa zamani au anakopelekwa.