#HABARI: Maelfu ya wananchi wamejitokeza kushiriki katika ziara ya Mwenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Singida, Ndugu Kenani L. Kihongosi, inayofanyika katika Wilaya ya Singida Mjini na Singida Vijijini.
Katika ziara hiyo, Ndugu Kihongosi amejikita kukagua uhai wa chama kuanzia ngazi ya mashina, kukagua utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo pamoja na kufanya mikutano ya hadhara kwa lengo la kusikiliza na kupokea kero, maoni na mapendekezo ya wananchi.
Wananchi wameonyesha mshikamano na imani kubwa kwa chama chao kwa kujitokeza kwa wingi katika mikutano hiyo, huku wakieleza changamoto zinazowakabili na kutoa pongezi kwa Serikali na CCM kwa utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika maeneo yao.
Ziara hiyo inaendelea leo katika Wilaya ya Mkalama, ambapo Mwenezi huyo anatarajiwa kuendelea na shughuli za kukagua uhai wa chama, kutembelea na kukagua miradi ya maendeleo pamoja na kuzungumza na wananchi kupitia mikutano ya hadhara.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
–
Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania