Wakulima mkoani Rukwa wameiomba serikali kuhakikisha inapeleka mapema mbolea, hususan ya kupandia, kabla ya kuanza kwa msimu wa kilimo ili kuendana na kalenda ya kilimo.
Maombi hayo yametokana na uhaba wa mbolea ya kupandia aina ya DAP, ambayo imeonekana kuwa pungufu kwa msimu huu kiasi cha kuwa tatizo kwa baadhi ya wakulima wakati wa kupanda mazao, huku serikali ikiendelea na jitihada za kuagiza mbolea hiyo kutoka nje ya nchi.
#AzamTVUpdates
Mhariri | John Mbalamwezi
(Feed generated with FetchRSS)