Wakulima wa Israel wameonya kuhusu “kuporomoka kwa mauzo ya nje ya bidhaa za kilimo kufuatia kuongezeka kwa kampeni za kimataifa za kususia bidhaa za Israel kutokana na vita vya Gaza.

Hayo yamo katika ripoti iliyoandaliwa na jarida la Marekani la Mondevis  ambayo inaeleza kinagaubaga changamoto mkubwa inayokabiliwa sekta ya kilimo ya Israel kutokana na bidhaa zinazotoka Israel kuendelea kususiwa katika maeneo mbalimbali ya dunia.

Ripoti hiyo inasisitiza kuwa, wakulima wa Israel wanakabiliwa na hasara kubwa na isiyo ya kawaida, na kwamba mauzo ya nje ya matunda na matunda ya jamii ya machungwa, hasa machungwa maarufu ya “Jaffa”, yamepungua sana huku masoko ya Ulaya yakifunga milango yao kabisa kwa bidhaa za Israel kwa sababu za kisiasa na kimaadili.

Ripoti hiyo inasema kwamba, baadhi ya masoko ya Ulaya yanakataa kukubali maembe kutoka Israel na matunda mengine ya machungwa isipokuwa katika hali ya uhaba mkubwa.

Maduka makubwa katika nchi kadhaa za Ulaya yameacha kuuza bidhaa za Israel ili kujibu ghadhabu za wanunuzi za bidhaa hizo kutokana na vita vya utawala wa Kizayuni dhidi ya Gaza.

Nchi nyingi duniani zinaendelea kujiunga na kampeni ya kususia bidhaa za utawala ghasibu wa Israel na vilevile za makampuni mengi ya Kimarekani yanayouunga mkono utawala huo wa kibaguzi ambao unaendelea kufanya mauaji dhidi ya wananchi wa Palestina hususan katika Ukanda wa Gaza.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *