#HABARI: Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo inapenda kuufahamisha umma na wadau wote wa michezo nchini kuwa, mchakato wa uchaguzi wa Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC) uliokuwa umetangazwa na uongozi wa TOC kufanyika tarehe 04 Oktoba, 2025 umesitishwa.
Uamuzi wa kusitishwa kwa mchakato huo wa uchaguzi umefanywa kwa mujibu wa Kifungu cha 27(2) cha Sheria ya Baraza la Michezo la Taifa (Marekebisho) Na. 6 ya mwaka 1971, pamoja na Kanuni za Usajili wa Vyama vya Michezo za mwaka 1999 Kanuni ya 11(6) na (7) ambao ulishafikishwa TOC kwa barua yenye Kumb. Na. BA.58/280/01/05 ya tarehe 30 Mei, 2025 na barua yenye Kumb. Na. CBA.52/280/01/01 ya tarehe 03 Septemba, 2025.
Uamuzi huo umetolewa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kufuatia kukataliwa kwa rufaa iliyowasilishwa na uongozi wa TOC kwa Mheshimiwa Waziri dhidi ya maamuzi ya Msajili wa Vyama vya Michezo.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @radioonetanzania
