
Rais wa Tume ya Ulaya Ursula Von der Leyen amesema kwamba umoja huo utaweka vikwazo kwa Israel na kusitisha sehemu ya biashara na nchi hiyo kutokana na vita vya Gaza.
Umoja huo wenye mataifa 27 umegawanyika pakubwa katika mtazamo wake kwa Israel naPalestinana bado haijulikani ikiwa mataifa hayo yataidhinisha kuwekwa kwa vikwazo hivyo na hatua za kuibana Israel kibiashara.
“Tutasitisha uungaji wetu mkono wa pande mbili kwa Israel. Tutasimamisha malipo yote lakini bila kuathiri kazi yetu na mashirika ya kiraia ya Israel au na taasisi rasmi ya kumbukumbu ya Israel ya wahasiriwa wa maangamizi ya Wayahudi -(Yad Vashem.) Pili, tutatoa mapendekezo mengine mawili kwa Tume ya Ulaya ambayo ni vikwazo kwa mawaziri wa Israel na walowezi wenye itikadi kali.Tutapendekeza pia kusitishwa kwa sehemu, Makubaliano yanayohusiana na biashara” amesema Ursula.
Ama katika hatua nyingine mashambulizi yaIsrael yamesababisha vifo vya watu 41 huko Gaza ambapo wizara ya afya ya Gaza imesema imepokea miili 41 ya watu hao waliouawa kwenye mashambulizi ya Israel katika muda wa saa 24 zilizopita. Watu wengine 184 wamejeruhiwa.
Jeshi la Israel limedai limefanya mashambulizi hayao kuwalenga wanamgambo wa Hamas.