Kikao hicho kilifanyika kwenye makao makuu ya  NATO  mjini Brussels siku ya Jumatano (Septemba 10), ambapo mabalozi wa mataifa 32 wanachama walijadiliana tukio hilo.

Waziri Mkuu wa Poland, Donald Tusk, aliliambia bunge la nchi yake kwamba kikao hicho cha Brussels kilifanyika chini ya Kifungu Nambari 4 cha Mkataba wa NATO, ambacho kinataka mazungumzo yafanyike haraka pale mwanachama mmoja anaposhambuliwa.

Katika tukio hilo la Jumanne (Septemba 9),  Poland  ikisaidiwa na ndege za kijeshi za Uholanzi ilifanikiwa kuzidunguwa baadhi ya droni hizo za Urusi.

Tukio hilo lilitokea siku tatu baada ya mashambulizi makubwa kabisa ya anga ya Urusi dhidi ya Ukraine tangu vita baina yao vianze.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *