Vijana wanataka uongozi bora na kuimarika kwa uchumi.

Sushila Karki waziri mkuu wa kwanza mwanamke Nepal aliye na umri wa miaka 73, alichukua nafasi hiyo baada ya maandamano ya vijana wa Gen Z kumuondoa madarakani mtangulizi wake Khadga Prasad Oli. Amepewa jukumu la kuirejesha nchi katika hali ya utulivu kuelekea uchaguzi mkuu ndani ya miezi sita ijayo.

Kabla ya kuanza rasmi majukumu yake alinyamaa kimya kwa dakika moja kuwakumbuka watu 72 waliuwawa katika maandamano hayo. Watu wengine 191 walijeruhiwa vibaya.

Maandamano hayo yalianza Septemba 8 baada ya serikali kufungia mitandao kadhaa ya kijamii. Baadae maelfu ya vijana hao waliojaa hasira waliteremka barabarani kupinga pia ufisadi na umasikini.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *