
Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala ndogo ya Dar es Salaam, inatarajia kutatoa uamuzi wa kuamua kama kesi ya uhaini inayomkabili mshtakiwa itafutwa, itarudishwa Kisutu au kuendelea Mahakama Kuu.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Uamuzi huu unatarajiwa kutolewa na jopo la majaji watatu (3), likiongozwa na Jaji Dunstan Ndunguru, huku majaji wengine wakiwa James Karayemana na Ferdinand. Jopo hili ndilo limepitisha masuala yote ya mapingamizi yaliyowasilishwa na Lissu.
Tundu Lissu amewasilisha mapingamizi mawili. Pingamizi la kwanza, ambalo tayari limesikilizwa, linahusu mamlaka ya Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam kusikiliza kesi yake, huku Lissu akidai kuwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu haikuwa na mamlaka ya kisheria kuendesha mchakato wa awali. Pingamizi la pili litasikilizwa baada ya Mahakama kutoa uamuzi juu ya pingamizi la kwanza; linalenga hoja yake kwamba Hati ya Mashitaka iliyotolewa Kisutu ni mbovu kisheria, haiwezi kuendelea bila marekebisho.
Tundu Lissu anakabiliwa na shitaka la uhaini kinyume na kifungu cha 39(2)(d) cha Sheria ya Kanuni za Adhabu, kilichotokana na maneno aliyoyatamka yanayohusiana na mpango wa kudhibiti au kuzuia uchaguzi mkuu wa 2025. Mashitaka haya yamevutia umakini mkubwa wa umma na vyombo vya habari, huku wananchi wengi wakisubiri kwa hamu uamuzi wa Mahakama Kuu: kuachiwa huru au kuendelea kusalia jela, jambo linaloangaliwa kuwa na athari kubwa kisiasa na kisheria nchini Tanzania.
Tundu Lissu alikamatwa Aprili 9, 2024, Mimba na kupelekwa Dar es Salaam. Siku iliyofuata, Aprili 10, 2024, alishitakiwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu