Israel na Marekani hazitoshiriki kwenye mkutanohuo unaofanyika New York. Uingereza, Canada na Australia zimekuwa nchi za kwanza kuitambua Palestina kama taifa.

Nchi nyingine kadhaa zikiwemo Ufaransa, Ubelgiji na New Zealand zimesema au zimeashiria kuwa zitaungana na mataifa mengine 150 ambayo tayari yanaitambua Palestina.

Matangazo ya kuitambua sehemu hiyo ya mashariki ya kati kama nchi huru yametolewa wakati Israel ikiendelea na kampeni yake ya kijeshi katika Ukanda wa Gaza.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *