
Mataifa hayo yamejiondoa ICC na kuiita mahakama hiyo yenye makao yake makuu mjini The Hague, Uholanzi, kama chombo cha ukandamizaji wa “ukoloni mamboleo” mikononi mwa mabeberu.
Viongozi wa kijeshi wa nchi hizo tatu waliounda Muungano wa Nchi za Sahel, AES, wamesema mahakama hiyo imejidhihirisha kuwa haina uwezo wa kushughulikia uhalifu wa kivita, uhalifu dhidi ya ubinaadamu, na uhalifu wa mauaji ya kimbari.
Nchi hizo pia zimesema zinataka kuanzisha taratibu za asili za kuimarisha amani na haki.
Dhamira ya mahakama hiyo iliyoanzishwa mwaka 2002 ni kuwashtaki watuhumiwa wa uhalifu mkubwa zaidi, kama vile uhalifu wa kivita, wakati ambapo nchi zinakosa nia au uwezo wa kufanya hivyo zenyewe.