Mkutano wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifaunaendelea hii leo ambapo viongozi mbalimbali wanatazamiwa kuendelea kutoa hotuba zao.
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky, Masoud Pezeshkian wa Iran na Ahmad al-Sharaa wa Syria wamepangwa kutoa hotuba zao mchana huu katika makao makuu ya umoja huo mjini New York, Marekani.
Mbali na hotuba za viongozi hao, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa linapanga pia kujadili hii leo namna ya kushughulikia mada ya akili mnemba (AI).
Itakumbukwa kwamba mzozo wa Mashariki ya Kati, vita vyaUrusi dhidi ya Ukraine,changamoto za kifedha za Umoja wa Mataifa ndio mada kuu katika mkutano huo uliowakusanya viongozi wa nchi na serikali 150.
