
Afisa mmoja wa serikali ya Iran amesema mabaharia tisa waliokuwa ndani ya chombo hicho wameokolewa.
Meli hiyo, iliyokuwa imebeba tani 2,500 za saruji nyeupe, ilikuwa safarini kutoka Ras Al Khaimah, Umoja wa Falme za Kiarabu, kuelekea Bandari ya Shuaiba nchini Kuwait, kabla ya kuanza kujaa maji karibu maili mbili kutoka Kish mnamo saa 7:30 mchana kwa saa za eneo hilo.
Shirika la Tasnim limesema nusu ya meli hiyo kwa sasa imezama na uchunguzi kuhusu chanzo cha kisa hicho unaendelea.