Aliyekuwa Katibu wa Chadema Mkoa wa Mwanza, Boniface Paul Mkobe Nzagamba, amejiunga rasmi na Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kupokelewa leo na Mgombea Urais wa CCM, Dkt. Samia Suluhu Hassan, katika mkutano wa kampeni uliofanyika Viwanja vya Nyamagana, Mwanza.
Nzagamba, ambaye pia aliwahi kuwa Katibu wa Baraza la Vijana Chadema kwa miaka kumi, amesema amejiunga na CCM baada ya kutokubaliana na misimamo ya chama chake cha zamani.
✍ @claud_jm
#AzamTVUpdates