Mkurugenzi wa zamani wa shirika la upelelezi la Marekani, FBI, James Comey, tarehe 8 Oktoba, ameripoti rasmi mbele ya mahakama ya shirikisho huko Alexandria, karibu na mji mkuu, Washington. 

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Na mwandishi wetu huko Atlanta, Edward Maille

James Comey amekana mashitaka yaayomkabili. Wakili wake ameelezea mashtaka yanayomkabili mteja wake kama “kulipiza kisasi.” Anakabiliwa na kifungo cha hadi miaka mitano jela. Kesi hiyo imepangwa kuanza mapema mwezi wa Januari. Comey alishtakiwa mwezi Septemba kwa kuzuia kamati ya uchunguzi na kusema uongo kwa Baraza la Congress. Comey amekuwa akikosolewa kwa muda mrefu na Donald Trump, na shtaka lake linaonekana na wengine kama shambulio la kisiasa.

James Comey alikuwa mkurugenzi wa FBI nchini Marekani wakati Donald Trump alipoingia madarakani kwa mara ya kwanza, na rais alimfuta kazi mwaka wa 2017 kwa sababu Comey alikuwa akichunguza iwapo kampeni ya uchaguzi wa urais ya Donald Trump ilishirikiana na Urusi kushawishi uchaguzi huo.

Mkurugenzi huyo wa zamani wa FBI tangu wakati huo amekuwa adui mkuwa wa Donald Trump, na shtaka hili linaonekana na baadhi ya wakosoaji wa rais kama shambulio la kisiasa na changamoto kwa uhuru wa mahakama. Wiki chache zilizopita, rais alimtaka Mwanasheria Mkuu Pam Bondi kuwafungulia mashtaka watu anaowaona kuwa maadui.

Wakati huo huo Mwendesha mashitaka wa Jimbo la New York Letitia James analengwa na Donald Trump. Hata hivyo, wiki chache zilizopita, mwendesha mashtaka mkuu ambaye alipaswa kumchunguza mkurugenzi wa zamani wa FBI na Mwanasheria wa Jimbo la New York alijiuzulu kwa shinikizo kutoka kwa Donald Trump, akibaini kwamba hakuwa na ushahidi wa kutosha wa kuwafungulia mashtaka. Mwendesha mashtaka huyu alibadilishwa na mfuasi wa rais.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *