Mgombea urais kwa tiketi ya CCM, Dkt. Samia Suluhu Hassan, ameahidi kukamilisha reli ya kisasa ya SGR kutoka Tanga hadi Musoma na kufufua bandari za Mkoa wa Mara ili kuchochea uchumi wa Kanda ya Ziwa.

Akizungumza Musoma Mjini, Dkt. Samia pia amesema serikali yake itapanua Uwanja wa Ndege wa Mara ili uweze kupokea ndege kubwa, hatua itakayoongeza biashara na utalii.

Ametoa wito kwa wananchi kuichagua CCM Oktoba 29 ili miradi hiyo mikubwa iendelee kuwanufaisha Watanzania.

✍ @claud_jm
#AzamTVUpdates

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *