Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Ridhiwani Kikwete amesema Maadhimisho ya Wiki ya Vijana Kitaifa 2025 yatazinduliwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.

Sambamba na hilo amesema uzinduzi wa maadhimisho hayo utafanyika katika viwanja vya Uhindini jijini Mbeya.

Kikwete amesema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa mikutano uliopo ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Mbeya.

Waziri Ridhiwani Kikwete amesema Wiki hiyo huadhimishwa kila Mwaka Oktoba 8 hadi 14 kwa kuwakutanisha vijana kutoka Tanzania bara na Visiwa kumuenzi Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Nyerere, kwa lengo la kujadiliana, kuonesha vipaji, bunifu na kazi wanazozifanya.

Imeandaliwa na @moseskwindi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *