#HABARI: Jeshi la Polisi Mkoa wa Ruvuma linaendelea na upelelezi wa tukio la kupotea kwa Padre Camillus Nikata wa Jimbo Kuu Songea, ambaye pia ni Mhadhili wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustino Tanzania (SAUT) Mwanza.
Akiongea Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma Kamisha Msaidizi Mwandanizi wa Polisi (SACP) Marco G. Chilya amesema kuwa Padri Nikata alifika Songea tarehe 03.10.2025 akitokea Dodoma, huku akiwa na Mhadhiri mwenzake ambaye ni Padre wa Jimbo la Songea na kufikia katika nyumba ya Mapadre, St. Shanney, Ilipofika tarehe 07.10.2025 majira ya jioni Father Nikata alionwa na Padre mwenzake huko Mtaa wa Kanisani akiwa na kibegi kidogo Mkononi akielekea Stendi ya zamani ya Mabasi Mfaranyaki ambapo tokea tarehe hiyo hakuweza kurudi mahali alipofikia jimboni.
Hata hivyo uongozi wa Kanisa hilo na Mapadre wenzake waliendelea na juhudi za kumtafuta sehemu tofautitofauti ambazo walisadiki kuwa atakuwepo lakini hawakufanikisha kumpata ndipo ilipofika tarehe 09.10.2025 waliweza kutoa taarifa ya kutoonekana kwa Father Nikata tangu tarehe 07.10.2025.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
–
📱Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 📱kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.