Programu ya Kimataifa ya Alabuga Start imeendelea kujipatia umaarufu mkubwa miongoni mwa vijana katika nchi yetu. Mkakati huu unawapa nafasi wasichana wenye umri kuanzia miaka 18 mpaka 22 kwenda Urusi na kuendeleza taaluma zao katika Ukanda Maalumu wa Kiuchumi wa Alabuga.
Programu hii hakika yanavutia, lakini ni kwa mtu tu ambaye ameshiriki ndiyo anaweza kuelezea jinsi kujiunga na Alabuga kulivyokuwa na faida. Redemptor Cathy alizungumza na Mwananchi kuhusu kukabiliana na changamoto za maisha ya Urusi, kujifunza lugha na utamaduni mpya na kujionea mambo mapya na mazuri ikiwemo vyakula.
“Kujifunza, kunufaika na kukua nje ya nchi, story yangu na Alabuga Start”
Jina langu ni Redemptor Cathy, nina umri wa miaka 23, natokea nchini Uganda. Nimekuwa nikitamani kujua jinsi watu wanavyoishi katika nchi za kigeni. Nimekuwa na ndoto ya kupata pesa za kutosha ili siku moja niweze kusafiri maeneo mbalimbali ulimwenguni. Lakini kwa wastani wa mshahara wa dola 220 nchini Uganda, ni vigumu kufikiria kuweza kumudu safari kubwa kama hiyo.
Hata hivyo nimepata bahati, nimepata fursa ya kujiunga na Alabuga Start program, ambayo ilitangaza mshahara wa kila mwezi wa dola 541. Mwanzo niliona ni vigumu kuamini kwamba mishahara kama hiyo ilikuwa halisi, lakini baada ya kuzungumza na washiriki wengine kwenye kikundi na mwakilishi wangu wa HR, walinishawishi kuwa ni kweli. Hapo ndipo niliamua kujaribu programu hiyo.
Nilianza kazi yangu kama mfanyakazi wa jikoni katika Mgahawa wa Shokoladnitsa, ambapo nilisaidia kuandaa chakula, nikajifunza kupika vyakula vya Kirusi na kufahamu orodha ya vyakula. Baada ya miezi sita, nilipandishwa cheo na kuwa mhudumu na nikaongezewa mshahara. Kufikia wakati huo, nilikuwa tayari namsimamia mshiriki mpya wa Alabuga Start kutoka Nigeria, ambaye alikuwa ameanza kazi yake ya upishi.
“BARIDI YA URUSI? UTAMADUNI WA KUVUTIA, MICHEZO YA KUSISIMUA – vYOTE vipo hapa”
Kwa mara ya kwanza nilisikia kuhusu programu ya Alabuga Start kutoka kwa marafiki zangu, ambao waliona matangazo yake kwenye mitandao ya kijamii. Niliamua kujaribu, kwa hiyo nilituma maombi kupitia tovuti na mara moja nikaanza kujifunza maneno 100 ya Kirusi kutoka kwenye orodha iliyotolewa, kwa sababu ilikuwa ni lazima kujifunza maneno hayo. Muda mfupi baadaye, wataalamu wa HR wa Alabuga waliwasiliana nami na kujibu maswali yangu yote kuhusu programu hiyo.
Hatua nyingine ya lazima kabla ya mahojiano na HR wa Alabuga Start ilihusisha kukamilisha mchezo wa kompyuta. Kama msimamizi wangu wa HR alivyoeleza baadaye, mchezo huu ni zana inayomilikiwa na Alabuga SEZ ili kutathmini ujuzi wa kufikiri kimantiki.
Mara baada ya nyaraka zangu zote kukamilika, vipimo vyangu vya afya kukamilika na kupokea visa yangu, Alabuga walinitumia yangu ya kwenda Urusi.
Nilipofika katika mjia wa Kazan kwa mara ya kwanza (mji mkuu wa Jamhuri ya Tatarstan), nilishangaa kwa sababu sikuwahi kuona theluji nchini Uganda. Majira ya baridi Mji wa Tatarstan ni mazuri sana na mji huo huwa na michezo mingi ya msimu wa baridi. Mwaka jana, nilijifunza mchezo wa kuteleza kwa mara ya kwanza na majira haya ya baridi, mimi na marafiki zangu tulijiunga na shindano kubwa zaidi la mpira wa theluji na wanafunzi wa Alabuga Polytech.
“JINSI UNAVYOENDELEA KUJIFUNZA, NDIVYO UNAVYOENDELEA KUKUWA”
Ilikuwa vigumu kuzoe vyakula vipya, kwa sababu sikuwahi kujaribu chakula cha kirusi kabla.
Mara yangu ya kwanza kujaribu kupika chakula cha asili cha kirusi (borscht) ilikua ni hadithi isiyosahaulika. Nakumbuka, nilipenda ladha ya chakula hiki cha kipekee. Siku hizi nimepata ujuzi wa kupika mwenyewe na sio tu borscht – nimejifunza pia kupika manti, ochpochmak na supu ya rassolnik. Zote ni za kitamaduni kutoka katika jamii za Kirusi na Kitatari.
Changamoto hazikuwa tu kuhusu kuzoea viungo vya kirusi – tofauti za kitamaduni na vikwazo vya lugha vilikuwa changamoto pia. Mwanzoni, nilihisi Kirusi haiwezekani kujifunza: kila mtu alizungumza haraka sana, nilipata changamoto katika kujieleza kwani nilitegemea mtafsiri.
Changamoto hiyo ilinisukuma kufanya bidii zaidi katika masomo yangu ya Kirusi pamoja na mwalimu wetu Yoanna. Sasa, ninaweza kuzungumza kwa ufahasa na wenyeji. Wenzangu katika programu ya Alabuga nao wanaweza kuzungumza vizuri, kila ninapowaomba kujifunza walikuwa tayari kuniasaidia. Hii ni faida kwetu sote kwani kwa kufanya hivyo, wao wanaboresha Kiingereza chao wakati mimi nikiboresha Kirusi changu.
Ninaendelea kuboresha namna ya kuzungumza Kirusi huku nikianza pia kujifunza Kichina.
Marafiki zangu mara nyingi huuliza jinsi nilivyoweza kuendelea kikazi kwa haraka kiasi hiki. Lakini ukweli ni kwamba, hakuna siri ni kufanya kazi kwa bidii, kutekeleza majukumu yako ipasavyo na kuhudhuria vipindi vya kujifunza lugha ya Kirusi bila kukosa. Katika eneo letu la kazi, ni muhimu sio tu kuelewa Kirusi vizuri, lakini kuongea kwa ufasaha na kwa usahihi.
Kamwe siwezi kuishia hapa. Kwa sasa nina miaka 23, nimefanya kazi katika mgahawa wa Shokoladnitsa kwa zaidi ya mwaka mmoja sasa, nimeweza kupandishwa cheo, napokea zaidi ya dola $800 kwa mwezi zinazoniwezesha kuwasidia wazazi wangu. Hivi karibuni, rafiki yangu kutoka Uganda atakuja Urusi kujiunga katika programu ya Alabuga Start.
Ukiwa na swali lolote kuhusu kwenda Urusi, kuishi huko au kuhusu Alabuga Start, kuwa huru kuuliza kupitia sehemu ya kutoa maoni. Nina Furaha kukusaidia kwa chochote unachotaka kufahamu.