Mamlaka ya Usafiri wa Anga nchini (TCAA) imewataka wataalamu wa sekta ya anga sambamba na watumiaji wa huduma za utafiti wa anga akiwemo mashirika na abiria wanaopanda ndege na watumiaji wengine wakiwemo waendeshaji wa ndege nyuki kutafuta ufafanuzi wa masuala ambayo wanahitaji taarifa zaidi.
Wito huo wa TCAA umetolewa na wasimamizi wa dawati la taarifa katika maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Wateja ambayo mwaka huu kitaifa ina kauli mbiu ya “Mission: Possible – Mpango Umewezekana.”
“Wataalamu na wadau mbalimbali wa usafiri wa anga wakiwemo marubani, wahandisi, wanafunzi na mashirika ya ndege wana mengi ya kujadiliana nasi kwa jailli ya kuendeleza kuiboresha sekta ya usafiri wa anga nchini na hii ni nafasi nzuri ili kukuza wigo wa ubora wa huduma na watumiaji wa huduma za usafiri wa anga nchini wakati huu ambapo sekta hii imeendelea kuwa kiungo muhimu cha ukuaji wa uchumi kupitia utalii na matumizi ya huduma nyinginezo” amesema Zuhura Lwamo Afisa Uhusiano na Mawasiliano Mkuu wa TCAA
Sekta ya usafiri wa anga nchini imeendelea kupiga hatua baada ya Chuo Cha Usafirishaji (NIT) kuidhinishwa na Wakala wa Usalama wa Anga wa Umoja wa Ulaya (EASA) kuwa Kituo cha Mafunzo na Mitihani ya Usafiri wa Anga.
Imeandaliwa na @moseskwindi