Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) umewakumbusha waajiri wanaosuasua kulipa michango ya wafanyakazi wao kuhakikisha wanalipa mara moja kabla ya kuchukuliwa hatua, ikiwemo kufikishwa katika vyombo vya sheria.
Kaimu Meneja wa NSSF Mkoa wa Mbeya, Meksal Salum ametoa wito huo wakati akizungumza na wanahabari, akisisitiza kuwa kutokulipa michango ya wafanyakazi ni kosa kisheria na kunawanyima haki zao za msingi.
#AzamTVUpdates
Mhariri | John Mbalamwezi