Utafiti unaofanyika katika mradi wa kimkakati wa Eyasi Wembere unaolenga kutafuta mafuta na gesi katika bonde la ufa la Afrika Mashariki umeonesha matumaini makubwa ya kupatikana kwa mafuta na gesi katika bonde hilo.
Hayo yamebainika wakati Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Dkt. James Mataragio alipofanya ziara ya kukagua maendeleo ya utekelezaji wa mradi huo mkoani Arusha wilaya ya Karatu.
Mhariri @moseskwindi