
Chama cha Democratic Party of Côte d’Ivoire (PDCI) na African Peoples’ Party – Côte d’Ivoire (PPA-CI), ambavyo viongozi wake hawakuidhinishwa kwenye uchaguzi wa urais, viliitisha maandamano Oktoba 11 huko Cocody, maandamano ambayo hatimaye yamepigwa marufuku. Kulingana na Wizara ya Mambo ya Ndani, watu 237 wamekamatwa Abidjan na wengine 18 huko Dabou, takriban kilomita 40 kutoka mji mkuu wa kiuchumi.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Na mwanahabari wetu mjini Abidjan, Abdoul Aziz Diallo
Asubuhi ya leo, Oktoba 11, barabaraba kuu ya Latrille, njia iliyopangwa ya maandamano ya “muungano”, imewekwa chini ya uangalizi mkali. Katika makutano ya Saint-Jean, wapita-njia wamekaguliwa kwa utaratibu, na jaribio lolote la kukusanyika lilizuiwa haraka.
Vijana kadhaa wamekamatwa, wakati mwingine kwa ukatili. “Ninakuja kuandamana kutafuta amani na ninaona watu waliovalia sare za jeshi wakichukua watoto kila mahali,” mwanaharakati amesema. “Yeyote anayekuja, anawawekwa kwenye gari la mizigo. Hatuwezi kuandamana.”
Kundi jingine la waandamanaji lilijaribu kukusanyika tena katika kitongoji cha Blockhaus, mitaa michache na eneo hilo. Lakini polisi waliingilia kati kwa mabomu ya machozi kutawanya umati huo. “Tunatazama mambo haya kwa moyo mzito,” alisema mkazi aliye karibu na upinzani. “Watu waliandamana huko Yopougon, maandamano yaliyopangwa vizuri, hakuna kilichotokea. Kwa hiyo, katika suala la maandamano, upinzani umekomaa sana; wawaache tu watu waandamane. Tunachokiona hapa ni ushenzi, vurugu zisizo na maana.”
“Kuandamana licha ya uwepo wa jeshi”
Waanzilishi wa maandamano hayo walipongeza uhamasishaji wa wanaharakati, huku wakitoa wito wa mazungumzo. “Watu walidhamiria kujitokeza na kuonyesha kutoridhika kwao licha ya uwepo huu wa kuvutia wa kijeshi,” amesema Sébastien Dano Djédjé, kiongozi mtendaji wa PPA-CI. “Serikali inaelekea kwenye uchaguzi ambao inaamini kuwa inaweza kuandaa kwa kishindo.”
Kwa upande wake, Waziri wa Mambo ya Ndani Jenerali Vagondo Diomandé anahakikisha kwamba vikosi vya usalama “walifanya kazi yao kwa njia ya kisheria na kwa kufuata sheria.” Wanaokamatwa, anaonya, watafikishwa katika mahakama husika kujibu kwa vitendo vyao.