
Maandamano dhidi ya serikali nchini Madagascar yanazidi kuongezeka. Siku ya Jumamosi, Oktoba 11, makundi ya wanajeshi yalijiunga na maandamano katika mitaa ya Antananarivo, na kikosi cha jeshi la Madagascar kilitoa wito wa “kukataliwa kwa amri ya kuwapiga risasi” waandamanaji. Shinikizo bado zinaendelea kwa Rais Andry Rajoelina. Kufikia Jumapili, Oktoba 12, asubuhi, hali ilikuwa bado haijafahamika.
Imechapishwa:
Dakika 2 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Kwa sasa haiwezekani kubainisha aliko Rais Andry Rajoelina. Hata hivyo, ofisi ya rais wa Madagascar imetoa taarifa asubuhi ya Oktoba 12 ili kushutumu “jaribio la kunyakua mamlaka kwa nguvu kinyume cha sheria linaloendelea sasa nchini Madagascar.” Ofisi ya rais inatoa wito kwa vikosi muhimu vya taifa kuungana ili “kutetea utaratibu wa kikatiba na mamlaka ya kitaifa.”
Hali ni ya sitofahamu kabisa
Jiji la Antananarivo limekuwa shwari kabisa asubuhi ya leo, anaripoti mwandishi wetu huko Madagascar, Sarah Tétaud. Usiku haukuwa na matukio. Lakini ni kweli kwamba bado ni vigumu kujua nani anashikilia kwa sasa uongozi wa nchi.
Jana, Jumamosi, Oktoba 11, mwito huu wa kukataa amri ya kuwapiga risasi waandamanaji, ambao ulifuatwa na makundi kadhaa ya askari, ulionyesha kwa wote kwamba hali ya kutoiamini serikali imeenea kote nchini. Hata hivyo, bado ni vigumu kusema kuwa ni mapinduzi, kwani, tangu wanajeshi walipozungumza moja kwa moja kutoka eneo la Mei 13i, hakujawa na matangazo mapya kutoka jeshi.
Changamoto iliyopo sasa ni kuona kama wito huu utazingatiwa na wanajeshi walio wengi, au iwapo kutakuwa na mgawanyiko ndani ya vikosi vyenyewe.
Asubuhi ya leo, Polisi ya taifa imebainisha kujitolea kwake kwa kwa raia. Katika video, shirikisho la Muungano wa polisi wa taifa hata hivyo limetoa changamoto kwa maafisa kuhusu hali zao za maisha na kazi ili kuhakikisha ulinzi wa raia. Kikosi cha askari ambacho kinatuhumiwa na waandamanaji kuwa nyuma ya ukandamizaji, bado hakijatoa tangazo lolote.
Capsat inadai kuchukua udhibiti wa vikosi vya jeshi la nchi hiyo
“Kuanzia sasa, maagizo yote kutoka kwa jeshi la Madagascar, iwe jeshi la nchi kavu, la anga, au wanajeshi , yatatoka katika makao makuu ya Capsat (Jeshi la Utumishi na Huduma za Utawala na Kiufundi),” wametangaza maafisa wa kikosi hiki katika taarifa ya video.
“Tuko hapa kulinda, sio kutisha,” kinabainisha kikosi cha askari (Gendarmerie)
Maafisa wa ngazi za juu zaidi wa kamandi ya Kitaifa ya Gendarmerie pia walizungumza katika hotuba iliyorekodiwa iliyorushwa kwenye mitandao ya kijamii, anaripoti mwandishi wetu huko Antananarivo, Sarah Tétaud. Wakikosolewa kwa matumizi yao ya nguvu dhidi ya waandamanaji, maafisa wanakiri baadhi ya dhuluma ndani ya askari wao na wanadai kuwa wamechukua hatua kushughulikia hili. “Tuko hapa kulinda, sio kutisha,” wanabainisha.
Leo asubuhi, vuguvugu la vijana la Gen Z kwa mara nyingine tena limeitisha maandamano katika mitaa ya mji mkuu. Sehemu ya maandamano hayo yalitarajiwa kuanza saa 5:00 mchana.