Madrid, Hispania. Real Madrid wamepokea habari njema kuelekea mechi yao ya LaLiga dhidi ya Getafe itakayopigwa Jumapili, Oktoba 19, 2025 baada ya kuripotiwa kuwa mshambuliaji Kylian Mbappe atakuwa tayari kucheza. 

Nyota huyo wa kimataifa wa Ufaransa amekuwa katika kiwango cha juu msimu huu, akifunga mabao 14 katika mashindano yote akiwa na Los Blancos.

Kwa mujibu wa Mundo Deportivo (kupitia Madrid Universal), Mbappe yupo fiti na yuko tayari kuwavaa Getafe, baada ya kujiondoa kwenye kikosi cha Ufaransa kilichoikabili Iceland katika mechi ya kufuzu kombe la dunia 2026.
 
Mbappe alifunga bao moja kwenye ushindi dhidi ya Azerbaijan wiki iliyopita kabla ya kupata majeraha ya kifundo cha mguu na kulazimika kutoka uwanjani dakika ya 83.

Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka amekuwa na mwanzo mzuri msimu huu akiwa na Real Madrid, akifunga mabao 9 katika mechi 8 tu za La Liga. Pia amefunga mabao 5 katika mechi 2 tu za Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu huu 2025-26.

Mbappe aliifungia Real Madrid bao katika ushindi wa 3-1 dhidi ya Villarreal kabla ya mapumziko ya kimataifa. Ingawa alitoka uwanjani akiwa anashikilia kifundo cha mguu wake wa kulia, alirejea kuchezea Ufaransa dhidi ya Azerbaijan.

MBAP 01

Kikosi cha Xabi Alonso kinatarajia kuendeleza ubabe wao kileleni mwa LaLiga watakapokutana na Getafe kwenye Uwanja wa Estadio Coliseum. Madrid imeshinda mechi 7 kati ya 8 za ligi msimu huu, ikipoteza mechi moja tu dhidi ya wapinzani wao wa jadi, Atletico Madrid.

Mbappe alishinda Kiatu cha Dhahabu cha Hispania pamoja na cha Ulaya msimu wake wa kwanza akiwa Real Madrid, ikiwa ni mafanikio makubwa katika maisha yake mapya nchini humo.

Atakuwa na lengo la kuendelea na kiwango chake bora mwishoni mwa wiki hii, huku klabu ikiwa imeweka mikakati kuhakikisha hana matatizo yoyote ya kiafya kabla ya mechi dhidi ya Getafe.

Wakati huohuo, Real Madrid imepokea habari nyingine nzuri baada ya beki Ferland Mendy kurejea uwanjani kwa mara ya kwanza tangu kupata jeraha miezi sita iliyopita. 

Kwa mujibu wa ripoti kutoka AS, beki huyo wa Ufaransa alipata majeraha ya misuli wakati wa fainali ya Copa del Rey dhidi ya Barcelona mwezi Aprili, dakika za mwanzo za mechi hiyo.

MBAP 02

Ripoti hiyo imeeleza kuwa Mendy alishiriki mazoezi ya kikosi kizima siku ya Jumanne kwa mara ya kwanza tangu apate jeraha hilo, ambalo awali lilitarajiwa kumweka nje kwa takribani wiki 12. Beki huyo wa kushoto alikamilisha mazoezi yote na sasa analenga kurejea dimbani katika mechi ya El Clasico dhidi ya Barcelona Oktoba 25, siku kumi kutoka sasa.

Mendy anatarajiwa kujiunga na kikosi kipya chini ya kocha Xabi Alonso, huku Alvaro Carreras na Fran Garcia wakionekana kuwa mbele yake katika nafasi ya kuanza. Beki huyo mwenye umri wa miaka 30 atakuwa na kazi ya kujitahidi kuonyesha uwezo wake ili kupata nafasi katika kikosi cha kwanza.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *