Kongamano la Kutokuwepo kwa Taka limeanza siku ya Ijumaa mjini Istanbul, likiandaliwa na Taasisi ya ‘Zero Waste’, iliyoanzishwa chini ya uangalizi wa mke wa Rais wa Uturuki, Emine Erdogan, kwa kushirikiana na Wizara ya Mazingira, Miji na Mabadiliko ya Tabianchi, pamoja na Wizara ya Kilimo na Misitu.

Mradi wa ‘Zero Waste’ ulianzishwa na Emine Erdogan, ambaye ni Mwenyekiti wa Baraza la Ushauri la Juu la Umoja wa Mataifa kuhusu ‘Zero Waste’ na pia Mwenyekiti wa heshima wa taasisi hiyo, kwa ushirikiano na Umoja wa Mataifa.

Kongamano hili linafanyika kwa mara ya kwanza mwaka huu, chini ya kaulimbiu: “Watu, Maeneo, Maendeleo”.

Mada kuu zitakazojadiliwa ni pamoja na kubadilisha sera kuwa vitendo, kupanua wigo wa suluhu, kuhamasisha ufadhili, na kujenga ushirikiano.

Wakati wa kongamano hilo la siku tatu, ambalo linahudhuriwa na washiriki kutoka nchi 104 na wadau wa kimataifa 118, vikao vya mijadala vitagusia mada kama vile maana ya “zero waste” (kutokuwa na taka kabisa), kanuni na sheria, fedha, taka za kikaboni, mustakabali wa mitindo ya mavazi, uchakataji, athari za akili mnemba (AI), teknolojia, na suluhisho mbalimbali.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *