Miongoni mwa nchi zilizo masikini duniani ni Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo licha ya kuwa na utajiri wa mali na maliasili Kipato cha wakazi wengi kwa ajili ya kujikimu ni chini ya dola mbili kwa siku hali inayowafanya kuishi kwenye kiwango cha umasikini.

Kila asubuhi, akina mama Mamicho na Charline wanaungana na wenzao katika shughuli za kuchimba mashimo na kusomba udongo na mchanga katika maeneo ya ujenzi katika mji wa Bukavu ili kupata pesa kidogo ya kukidhi mahitaji ya familia zao. Waume zao hawana kazi; wengine wamekwenda kuchimba madini kwa muda sasa, lakini hawajawahi kutuma chochote nyumbani. Wanawake hawa wanakabiliwa na hali ya umaskini.

Siku ya Wakimbizi Duniani 2025 | Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo | Wakimbizi
Mwanamke aliyekimbia makazi, pamoja na watoto wake, wakiwa wamebeba baadhi ya mali zake zilizopatikana kutoka eneo ambalo zamani kulikuwa na kambi ya wakimbizi wa ndani (IDP) kabla ya kuharibiwa, huko Goma mnamo Februari 1, 2025.Picha: MICHEL LUNANGA/AFP/Getty Images

Asilimia 85 ya Wakongo hutumia chini ya dola 3 kwa siku

Kulingana na ripoti ya Benki ya Dunia iliyochapishwa Oktoba, 2025, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo inashika nafasi ya kwanza duniani kwa umaskini uliokithiri. Ripoti hiyo inaonesha kwamba asilimia 85.3 ya Wakongo kipato chao ni chini ya dola 3 kwa siku, hiki kikiwa kiwango cha chini zaidi duniani.

Ripoti ya Benki ya Dunia inabainisha sababu nyingi za umaskini nchini Kongo zikiwa ni pamoja na utawala mbaya, ufisadi; changamoto za kiuchumi; migogoro inayoendelea Mashariki mwa nchi hiyo; na upatikanaji mdogo wa huduma za msingi za kijamii kama vile elimu na afya.

Wachambuzi: Vita vya Mashariki mwa Kongo vyachangia

DR KONGO 2022 l Jiwe la Kobalti
Baadhi ya watu 20,000 wanafanya kazi huko Shabara, kwa zamu ya 5,000 kwa wakati mmoja. Kongo ilizalisha asilimia 72 ya cobalt duniani mwaka jana, kulingana na Darton Commodities.Picha: JUNIOR KANNAH/AFP/Getty Images

Akitathmini hali ya umaskini Kongo, mjumbe wa Shirika linalopambana na umaskini linaloitwa “ATD Quart Monde”, Daniel Alingilya anahisi kwamba vita mashariki mwa Kongo vimechangia pakubwa kuzorotesha maisha ya Wakongo

Naye mwanasheria, Maurice Mirindi ambaye ni naibu msemaji wa Shirika la kiraia katika jimbo la Kivu kusini anatarajia kwamba umaskini unaweza kutokomezwa nchini Kongo ikiwa kutakuwepo hata kiwango kidogo cha utashi wa kisiasa.

Benki ya Dunia imetoa wito kwa mamlaka ya Kongo kuharakisha mageuzi ya kimuundo, kuimarisha uwazi katika usimamizi wa umma na kuhamasisha uwekezaji katika sekta za uzalishaji. Kulingana na taasisi hiyo ya kimataifa ni mkakati unaolenga kuunda ajira na kuendeleza mtaji wa watu ambao utaweza kuwaondoa wakazi wa Kongo kutoka katika umaskini.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *