Uelewa mdogo kuhusu njia sahihi za kujikinga dhidi ya magonjwa yasiyoambukiza umetajwa kuwa chanzo cha ongezeko la magonjwa hayo, ambapo kwa mujibu wa takwimu za Shirika la Afya Duniani (WHO) kwa mwaka 2020, magonjwa yasiyoambukiza yalichangia zaidi ya vifo milioni 41, sawa na asilimia 71 ya vifo vyote duniani, ikilinganishwa na vifo milioni 57 vilivyorekodiwa mwaka 2016.
Kutokana na hali hiyo, wataalam wa afya wanahimiza jamii kuzingatia mlo bora na ufanyaji wa mazoezi ya mara kwa mara kama njia muhimu ya kupunguza hatari ya kupata magonjwa hayo.
#AzamTVUpdates
Mhariri | John Mbalamwezi