Video ya UNMISS iliyotumwa makao makuu ya Umoja wa Mataifa imeonesha tukio la viongozi wakikabidhi vifaa vya shule kwa watoto walioachiliwa kutoka jeshi la serikali.

Siku hiyo ni ya matumaini makubwa mjini Yambio, jimbo la Equatoria Magharibi nchini Sudan Kusini kwani watoto waliopoteza utoto wao vitani, sasa wanaupokea tena, wakiwa na ndoto mpya za elimu na maisha bora zaidi.

Hafla ya makabidhiano iliyofanyika kwa ushirikiano kati ya Jeshi la serikali na Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini humo (UNMISS), imeashiria azma ya serikali ya kuondokana na utumikishaji wa watoto jeshini.

Brigedia Akech Maker, Kamanda wa Kikosi cha 16 cha SSPDF, anasema “Hatutaruhusu watoto kujiunga na jeshi. Watoto wanaoonesha nia, tutawaelekeza kwenye elimu, na taasisi ziwaunge mkono ili wasirudi kambini.”

Afisa wa Ulinzi wa Watoto UNMISS,, Rita Bampo, akatoa ahadi akisema watoto lazima warejee kwenye jamii, na kwamba 

Tutahakikisha mchakato huu unafanikiwa na hakuna atakayewarudisha kwenye makundi ya kijeshi. Viongozi wote wahakikishe watoto wanapelekwa kwa mashirika yanayohusika.”

UNICEF pia imetoa huduma za kisaikolojia na vifaa vya kujifunzia kwa watoto hao, kuwasaidia kuanza upya safari yao ya elimu na matumaini.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *