Amesema vurugu za kijinsia zimeongezeka kwa karibu asilimia 90 ndani ya miaka miwili, na zaidi ya wanawake milioni 675 wanaishi karibu na hatari ya mapigano.
Robo ya karne baada ya Baraza la Usalama kupitisha azimio la kihistoria linalotaka uwakilishi bora wa wanawake katika mchakato wa amani, Guterres ameweka wazi uchunguzi kwamba kumekuwa na “Mkwamo na hata kurudi nyuma katika miaka mitano iliyopita”.
Kulingana naripoti hiyo, iliyochapishwa leo, dunia sasa ina idadi kubwa zaidi ya migogoro hai tangu 1946.
Jumla ya wanawake milioni 676 wanaishi ndani ya kilomita 50 kutoka maeneo yenye migogoro hatari, ikiwa ni kiwango cha juu zaidi tangu miaka ya 1990.
Vifo vya raia miongoni mwa wanawake na watoto vimeongezeka mara nne ndani ya miaka miwili, kutokana na vita visivyo na kikomo ambapo kanuni za kibinadamu hazufuatwi.
“Ukatili mkubwa uliofanywa dhidi ya wanawake na wasichana nchini Afghanistan, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC, Haiti, Myanmar, Sudan na Eneo la Palestina lililokaliwa kimabavu na Israel unaonesha hatari kubwa wanazokabiliana nazo,” aameandika Katibu Mkuu katika ripoti hiyo.
Wanawake wamekutana Sudan kujadili amani na haki za binadamu
Vita hadi ndani ya miili ya wanawake
Takwimu ni za kutisha kwa mujibu wa ripoti, kesi zilizoorodheshwa za ukatili wa kijinsia zinazohusiana na migogoro zimeongezeka kwa asilimia 87 ndani ya miaka miwili. Nchini Haiti, zaidi ya mara tatu ya vurugu zilizoripotiwa ni za ukatili wa kijinsia.
Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC ripoti nchi ambayo imekuwa kitovu cha vurugu duniani, kesi 38,000 ziliripotiwa katika jimbo la Kivu Kaskazini pekee katika miezi ya mwanzo ya mwaka huu, kufuatia shambulio la waasi wa M23 katika eneo hilo.
Ripoti pia inazungumzia mkusanyiko wa athari kwa wanawake wajawazito na vikwazo vya upatikanaji wa huduma za afya kama “ukatili wa uzazi”, ikikumbusha kuwa vitendo kama hivyo vinaweza kuhesabiwa kama kosa la jinali la mauaji ya kimbari wakati vinakusudia kuzuia uzazi ndani ya kikundi fulani. Nchini Gaza, mamia ya uzazi unafanyika “katikati ya vumbi, bila dawa za ganzi, huduma baada ya kujifungua, au maji.”
Ripoti inasisitiza kuwa ukatili huu si ajali yu bali umegeuka kuwa silaha ya vita, kama vile bunduki za mashambulizi.
Angel Musiime, afisa wa kata na mpatanishi wa amani katika wilaya ya Kyegegwa iliyopo magharibi mwa Uganda
Kutojumuishwa katika mazungumzo ya amani
Wakati mabomu yanapopiga, wanawake wanaendelea kuwekwa mbali na mazungumzo ambayo yanapaswa kuwaweka kimya.
Tano kati ya sita ya michakato ya mazungumzo hayajumuishi wanawake kabisa. Kwa wastani, wanawake wanawakilisha asilimia 7 ya wadau wa mazungumzo, asilimia 14 ya wadhamini na asilimia 20 ya walio saini makubaliano ya amani.
Kati ya makubaliano 36 yaliyofikiwa kwa jumla mwaka 2024, 11 tu yalihusisha wanawake au suala la jinsia.
“Vituo vya serikali, meza za mazungumzo ya amani na taasisi za usalama bado vinatawaliwa na wanaume, mara nyingi bila uwajibikaji halisi kwa matokeo ya maamuzi yao,” amesema Bwana Guterres.
Hata hivyo, utafiti unaonesha kuwa wanawake wanaposhiriki, makubaliano ya amani yanakuwa endelevu zaidi.
Wanawake na wasichana wanavuka mpaka wa Islam-Qala, na kuingia Afghanistan.
Dunia ina silaha zaidi na wanawake walipa gharama
Wakati huo huo, kuongezeka kwa mashambulizi ya kijeshi kumeshika kasi. Matumizi ya kijeshi duniani yalifikia dola trilioni 2.7 mwaka jana, ongezeko la asilimia 9.4 ikilinganisha na mwaka uliopita ikiwa ni ongezeko kubwa zaidi tangu kumalizika kwa vita baridi
“Njia ya amani si kupitia ukusanyaji wa silaha, bali kupitia uwekezaji katika zana za amani, kutimiza haki na maendeleo endelevu,” inasema ripoti.
Tofauti ni kubwa kwani chini ya asilimia 0.4 ya misaada ya kibinadamu katika muktadha wa migogoro inafikia mashirika ya wanawake. Dunia inatumia trilioni za dola kwa vita, na mabaki ni kwa wale wanaoteseka na matokeo yake.
Walinda amani katika mtihani
Operesheni za kulinda amani zinajaribu kulinda uwiano huu hatarishi. Uwiano wa wanawake katika vikosi umeongezeka zaidi ya mara mbili tangu 2018, kufikia zaidi ya asilimia 10.
Lakini operesheni nyingi, kama MONUSCO nchini DRC, imekumbwa na ongezeko la vurugu dhidi ya wanawake. Tatizo hili linaendelea, na hata kuongezeka, mwishoni mwa muda wa operesheni.
“Kuondolewa kwa operesheni kumeacha pengo la usalama linalowafanya wanawake na wasichana kuwa hatarini zaidi,” imeanisha ripoti hiyo.
Washiriki wa warsha kuhusu masuala ya misimamo mikali huko kambi ya wakimbizi ya Daadab nchini Kenya.
Mwanga wa kisiasa usio na matumaini
Mabadiliko machache ya kimfumo, uchaguzi wa wanawake marais nchini Mexico, Namibia na North Macedonia haujabadilishi chochote. Zaidi ya nchi mia moja hazijawahi kuwa na mwanamke kiongozi, na wanawake sasa wanaongoza nchi 29 tu.
Kamati ya Kuondoa Ubaguzi Dhidi ya Wanawake (CEDAW), chombo cha Umoja wa Mataifa kinachohusika na kufuatilia utu kwa haki za wanawake, kinabainisha kuwa kiwango cha uwakilishi cha asilimia 30 hakichukuliwi tena. Usawa kamili ndiko kunakohakikishia usawa wa kweli.
Mapinduzi ya takwimu za kijinsia yahiitajika
Suala kuu, lenye unyenyekevu zaidi, ni uzalishaji wa takwimu. Katibu Mkuu anataka “mapinduzi yatakiwmu ya jinsia kuelewa mahitaji na uzoefu wa wanawake katika maeneo ya vita, usalama, afya, haki na maisha”.
Hivi sasa, asilimia 15 tu ya fedha za uzalishaji wa takwimu zinahusu jinsia.
Bila takwimu sahihi, Guterres ameonya kwamba wanawake wanabaki kuwa wasioonekana katika sera za umma na kurudi nyuma, ambako hakuwezi kupimika, na kunaendelea.
Wanawake nchini Kenya
Tahadhari iliyo bayana
Kwa lugha yake ya kiasasi, maandiko hayo yana nguvu ya mashtaka. “Dunia ipo wakati ambapo mgawanyiko wa kisiasa una hatari ya kufuta miongo ya maendeleo.
“Ukimya na kutochukua hatua kutaacha mifumo hii iendelee,” ameonya Katibu Mkuu.
Miaka ishirini na tano baada ya matumaini yaliyozaliwa na ahadi ya dunia yenye usawa zaidi, ripoti hii inatoa tahadhari, wanawake hawadai tu ahadi, wanadai ahadi hizo ziheshimiwe.