Katika taarifa iliyotolewa leo na  timu ya Umoja wa Mataifa nchini Yemen timu hiyo imesema imesema wafanyakazi wake 15 wa kimataifa sasa wana uhuru wa kuzunguka ndani ya kituo hicho na wako katika mawasiliano na ofisi zao na familia zao. Wafanyakazi watano wa kitaifa wa Yemen, waliokuwa wamekamatwa tangu 18 Oktoba, pia wameachiliwa.

Taarifa hiyio imeongeza kuwa “Askari wa usalama wa Ansar Allah wameondoka kwenye kituo hicho cha Umoja wa Mataifa huko Sana’a,” ikionesha kumalizika kwa tishio la moja kwa moja kwa wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa.

Changamoto kwa mashirika ya kibinadamu

Tukio hili limetokea huku mvutano ukiendelea katika mji mkuu wa Yemen, ambapo mashirika ya kibinadamu yamekumbana na changamoto za kufanya kazi kwa usalama kutokana na vizuizi na matukio ya usalama mara kwa mara. Umoja wa Mataifa umekuwa ukitaka mara kwa mara uwepo wa uhuru wa mashirika hayo kutoa msaada wa kuokoa maisha kwa wananchi walioathirika na mgogoro wa muda mrefu wa nchi hiyo.

Uthibitisho wa Umoja wa mataifa wa kuachiliwa kwa wafanyakazi wake unadhihirisha azma ya shirika hilo kulinda wafanyakazi wake huku likiendelea na shughuli za kibinadamu nchini Yemen, nchi ambayo bado ipo kwenye  mojawapo ya migogoro mikubwa ya kibinadamu duniani.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *