Iliwashutumu waasi hao kwa kuwafukuza wakazi, kubomoa makanisa na kutumia mafundi wa Rwanda kuchukuwa data za kijiolojia ili kuanza tena na kupanua uchimbaji madini. “Kuna zaidi ya wafanyakazi 150 waliosalia’’.

Hatuwezi kuwasiliana nao,” kampuni hiyo ilisema. Serikali ya Rwanda haikujibu mara moja ombi la kutoa maoni.

Mashambulizi ya ndege zisizo na rubani mnamo Oktoba 15 yaliharibu miundombinu ya kuzalisha umeme kwenye mgodi huo.

Haijabainika ni nani alihusika na shambulio hilo la ndege zisizo na rubani. Mapigano mashariki mwa Congo yamesababisha vifo vya maelfu ya watu na kuwafanya maelfu wengine kuyahama makazi yao mwaka huu.

Makundi yenye silaha yameteka maeneo kadhaa ya uchimbaji madini mashariki mwa DRC yenye utajiri mkubwa wa madini, kulingana na wachunguzi wa Umoja wa Mataifa.

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa mwaka jana lilisema waasi wa M23 walikuwa wakipata karibu dola 300,000 kila mwezi kutokana na ushuru wa madini katika eneo lenye utajiri wa madini ya coltan, Rubaya.

Rais wa Marekani Donald Trump aliafiki makubaliano ya amani kati ya DRC na Rwanda mwezi Juni kama sehemu ya juhudi za kuleta utulivu mashariki mwa Congo na kuleta uwekezaji wa madini kutoka mataifa ya Magharibi.

Rwanda imekuwa ikikanusha kuwaunga mkono waasi wa M23, licha ya madai ya mara kwa mara kutoka kwa wataalamu wa Umoja wa Mataifa na serikali za kikanda.

Qatar imekuwa mwenyeji wa mazungumzo ya moja kwa moja kati ya DRC na M23.

Pande hizo mbili zilikosa kufikia muafaka kufikia muda wa mwisho wa kufanya hivyo Agosti, ikiwa ni makubaliano ya amani kama sehemu ya mchakato huo lakini mnamo Oktoba 14, walikubaliana na utaratibu wa ufuatiliaji wa kusitishwa kwa mapigano.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *