Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Morogoro, Rose Ebrahim, amewahimiza watumishi wa mahakama katika kanda hiyo kuendelea kusimamia na kuzingatia misingi ya kazi yao, huku wakitimiza wajibu wao kwa uadilifu ili kulinda amani na utulivu katika jamii.

Kauli hiyo ilitolewa wakati wa kufungua mafunzo ya siku mbili yaliyolenga kuongeza ufanisi wa kimahakama kupitia uelewa wa mabadiliko ya sheria. Jaji Ebrahim alisema kuwa ni muhimu kwa watumishi wa mahakama kuelewa majukumu yao kikamilifu ili waweze kuyatimiza kwa usahihi na kwa weledi.

✍Alpha Jenipher
Mhariri | @claud_jm

#AzamTVUpdates

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *