Ofisi ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Masuala ya Wanawake (UN women) ya Eneo la Afrika Mashariki na Kusini imefanya kazi kwa bidii kubadilisha hali hii. Ikiungwa mkono na mfumo wa kimataifa wa kubadilisha mtazamo wetu na kuunda sera za huduma za kujitunza, lengo ni rahisi kutoa thamani inayostahili huduma za kujitunza na kuzichukulia kama jukumu la kila mtu.
“Sekta ya huduma za kujitunza ni uti wa mgongo wa jamii zetu. Tunapowekeza katika huduma hizi, tunawekeza katika haki za kiuchumi, jamii imara, na mustakabali ambapo muda na vipaji vya wanawake vinathaminiwa kwa usawa.” Anasema Anna Mutavati, Mkurugenzi wa UN Women Mkoa wa Afrika Mashariki na Kusini.
Jinsi UN Women inavyojenga suluhisho za huduma Afrika
Mwaka 2022, UN Women imewaleta pamoja serikali, vyama vya wafanyakazi na watoa huduma jijini Nairobi kwa ajili ya maonesho ya sekta ya huduma katika ukanda huo. Kilichoanza kuwa mkutano sasa kimekua mtandao unaotengeneza suluhisho zinazogusa maisha ya kila siku: mashambani, masoko, maeneo ya kazi, nyumba na vijiji.
Kuanzia kwa upatikanaji rahisi wa maji na huduma za kulea watoto, hadi mafunzo mapya na ulinzi kwa watoa huduma za, mabadiliko yanashika kasi kupitia sheria mpya, bajeti, na kusaidia serikali kutambua huduma hizi kama huduma muhimu, si kazi za pembeni au zisizoonekana.
Saa zilizokuwa zimepotea kutembea kwa ajili ya kupata maji au kupika juu ya majiko yenye moshi sasa zimepatikana kwa ajili ya kujifunza, kupata kipato, au kupumzika. Wanawake wanahifadhi muda na kutumia saa hizo kuanzisha biashara, kujiunga na vikundi vya ushirika, na kuchukua nafasi mpya katika sekta ya huduma za kujitunza.
Nyumbani na katika vijiji, mazungumzo polepole yanabadilisha matarajio, huku wanaume wengi wakijiingiza kusaidia kazi za kila siku, kupunguza migogoro ya familia, na kuweka mfano mzuri kwa vizazi vijavyo. Hapa chini ni mifano mitatu ya jinsi mabadiliko haya yanavyoonekana katika maisha halisi.
Rwanda: Huduma za kulea watoto, majiko safi, na huduma za kujitunza kutambuliwa kisheria
Katika Gikomero, Marie Louise, mjane, awali alikuwa anatembea kwa masaa mengi kuvua maji, jambo lilimwacha amechoka na hana nguvu za kuangalia biashara yake ya mboga na wajukuu wake. Tanki la kuhifadhi maji ya mvua lililowekwa na UN Women lilikuwa suluhisho kubwa.
“Ninaweza kulima zaidi, kuuza zaidi, na kuwalea vizuri wajukuu wangu,” anasema.
Wasichana wakiwa katika mafunzo ya Roboti Rwanda
Rwanda imechanganya suluhisho za vitendo na mabadiliko makubwa ya kisheria. Mnamo Julai 2024, nchi hiyo imerekebisha sheria ya watu na familia kutambua kazi ya kulea au kuhudumia isiyolipwa katika mali za ndoa, ikitoa thamani ya asilimia 10–39 ya mali zilizopatikana kwa pamoja. Hii ilikuwa hatua muhimu yaUN Women kuthibitisha kuwa wanawake hutumia saa 3.7 kwa siku kwenye kazi za kutunza familia isiyolipwa, zaidi ya mara tatu ya wanaume.
Kwa kuandika huduma za kujitunza kisheria, Rwanda imetoa ishara wazi kwamba kazi isiyoonekana inayoshikilia familia na jamii ni kazi halali, na inahesabiwa.
Katika jamii, miundombinu ya kuokoa muda imeenea, zaidi ya meko 1,100 zinazotumia nishati kwa ufanisi na tanki 92 za maji ya mvua zinarahisisha shughuli za kila siku. Utafiti wa 2025 umeonesha wanawake walitumia saa walizohifadhi kulima, kuendesha biashara ndogo ndogo, na kuhudhuria mafunzo, kaya pia ziliona faida za kiafya kutokana na kupika kwa usafi zaidi.
Rwanda pia imebadilisha mtazamo wa nani anayefanya kazi za uangakizi wa familia. Katika maeneo ya Nyaruguru, Ngoma na Kirehe, vituo vipya vya maendeleo ya utoto wa awali vinatoa mahali salama pa kujifunzia na kustawi, huku wauguzi waliopata mafunzo wakizingatia lishe na kujifunza kwa watoto. Akina mama wanapata saa muhimu za kufanya kazi na kupumzika, na wanawake wa jamii wanapokea nafasi za kazi zinazolipwa kama wauguzi wa kitaalamu.
Mtazamo umebadilika pia. Kampeni ya uhamasishaji ya UN Women inayotangazwa kwenye redio na televisheni inahamasisha wanaume na wavulana kushiriki kazi za nyumbani. Katika utafiti wa hivi karibuni, asilimia 98 ya kaya ziliripoti ushiriki mkubwa wa wanaume katika huduma za kulea. Na kuimarisha maendeleo haya, Rwanda inaingiza huduma za kulea katika fedha za umma kwa kutumia Zana ya UN Women ya Kuendeleza Nafasi za Fedha za Kijinsia hivyo tanki za maji, meko safi na vituo vya kulea watoto si majaribio tu, bali hali mpya ya kawaida. Kazi hii inasaidiwa na Serikali ya Ujerumani, Wizara ya Ushirikiano wa Kiuchumi na Maendeleo (BMZ).
Vituo vya malezi ya watoto nchini Tanzania husaidia kupunguza muda ambao wanawake hutumia kuwahudumia watoto, hivyo kuwawezesha kushiriki katika shughuli nyingine za uzalishaji.
Tanzania: Wanawake wanapata saa, afya, na fursa mpya
Ikungi (mkoa wa Singida), Khadija Abdallah awali alitumia saa nyingi kukusanya kuni na kupika juu ya jiko lenye moshi. Kazi hizi zilimwachia muda kidogo kwa ajili ya duka lake na watoto. Lakini leo, kwa jiko lililoboreshwa iliyoletwa kupitia mpango wa UN Women unaounga mkono Serikali ya Kanada, kila kitu kimebadilika.
Mnamo mwaka 2021, Serikali ya Tanzania iliahidi kupunguza kazi za kulea zisizolipwa kwa wanawake, kupanua huduma za kijamii, na kuunda ajira za huduma za kujitunza zinazolipwa. Ahadi hizo sasa zimesaidiana na sera kama Sera ya Taifa ya Jinsia na Maendeleo ya Wanawake (2023), inayosisitiza uwajibikaji wa pamoja kwa huduma za kujitunza, na Mkakati wa Kitaifa wa Kupika Safi, unaolenga kaya asilimia 80 zitumie suluhisho safi kufikia 2034.
Mabadiliko yanaonekana wazi. Kote Singida, Dodoma na Zanzibar, zaidi ya teknolojia 400 za kupikia safi na nishati ya jua zimegawiwa, kupunguza muda wa kupika kwa hadi saa tatu kwa siku, na kupunguza kukusanya kuni kila wiki. Ikungi pekee, kaya 248 sasa zinatumia meko bora na wanawake waliofundishwa kuzisanikisha wanaongoza makundi mapya ya biashara chini ya mradi wa UN Women unaounga mkono Wizara ya Mambo ya Nje, Biashara na Maendeleo ya Kanada.
Huduma za kulea watoto sasa ziko karibu zaidi na mahali wanawake wanavyofanya kazi. UN Women ilisaidia uzinduzi wa vituo viwili vya kulea watoto katika maeneo ya masoko Ikungi na Puma kuwaruhusu wafanyabiashara kupata kipato wakati watoto wanajifunza kwa usalama. Zaidi ya vituo 3,000 vya Maendeleo ya Utoto wa Awali vimefunguliwa bara na 54 Zanzibar, pamoja na vyumba vipya vya kuwahudumia watoto wachanga katika ofisi na masoko vinavyofadhiliwa na mchango wa Serikali ya Tanzania kwa mpango wa UN Women wa Generation Equality.
Mitazamo pia inabadilika nyumbani. Mazungumzo ya jamii na kampeni zinafanya wanaume wengi kushiriki kazi za nyumbani. Matokeo yake, Ikungi na Puma wanawake wameripoti ratiba za maisha zenye usawa zaidi na shinikizo la muda kupungua.
Na muhimu zaidi, suluhisho za huduma za kujitunza zinafikia wale waliokuwa wakipuuzwa mara kwa mara. Kwa wanawake wenye ulemavu, huduma mpya zinazoungwa mkono na Serikali ya Canada zinamaanisha uhuru mkubwa, heshima, na fursa ya kushiriki kikamilifu katika maisha ya kijamii.
Afrika Kusini: Watoa huduma wanapolindwa, kila mtu anafaidika
Cape Town, Noluthando, mfanyakazi wa huduma za nyumbani, amekuwa akiwalea watoto, watu wazee, na nyumba kwa zaidi ya miaka 15, mara nyingi bila mkataba, likizo iliyolipwa, bima ya afya, au kinga yoyote.
“Sisi ndio mikono inayoshikilia familia pamoja, lakini kwa muda mrefu tumekuwa wasioonekana,” anasema.
Afrika Kusini ina jumla ya wafanyakazi wa huduma za nyumbani milioni 1.2, wengi wao wakitoka jamii za kipato cha chini, wahamiaji na jamii zilizokuwa zikipuuzwa kihistoria. Kwa miongo kadhaa, kazi yao iliwasaidia kaya na uchumi wa taifa huku ikibaki gizani, isilindwe na kupunguzwa malipo.
Maafisa wakiwa katika picha ya pamoja baada ya warsha ya polisi inayozingatia jinsia nchini Afrika Kusini, Desemba 1, 2023.
Mabadiliko sasa yanaanza kuonekana. Mnamo 2022, Afrika Kusini ilianzisha Sheria ya wafanyakazi wa huduma za nyumbani, kuweka viwango vya chini vya malipo na ulinzi kazini. Shinikizo kutoka vyama vya wafanyakazi pia limepata haki ya kujiunga na Mfuko wa Bima ya Ajira kutoa msaada wa kifedha wa muda mfupi kwa wafanyakazi wanapopoteza kazi.
Kwa kushirikiana na vyama vya wafanyakazi, UN Women ilizindua kampeni, mafunzo, na warsha katika mikoa ya Gauteng, Western Cape na KwaZulu-Natal. Juhudi hizi zinawawezesha wafanyakazi kujua haki zao, kujisajili kwa ajili ya manufaa, na kuhimiza utekelezaji mzuri wa sheria za kazi. Vipaumbele vyao ni wazi: usajili wa lazima kwa wafanyakazi wote wa huduma za nyumbani (pamoja na wahamiaji), kuleta viwango vya mshahara vinavyolingana, ukaguzi bora wa kazi, na zana rahisi za kuripoti.
Kama Mwenyekiti wa G20 mwaka 2025, Afrika Kusini inaleta ujumbe huu duniani kote: uchumi unarejea haraka zaidi wakati huduma za kujitunza zinathaminiwa, na watoa huduma wanapolindwa.
Nini hubadilika tunapowekeza katika huduma za kulea?
· Umaskini wa muda unashuka- kupikia kwa kutumia nishati kidogo, vyanzo vya maji safi vilivyo karibu, na saa za bure za kulea watoto kila siku kwa ajili ya kupata kipato, kusoma au kupumzika.
· Mapato yanarudi- wanawake huanzisha biashara, kujiunga na ushirika na kupata ajira zilizolipwa.
· Wanaume wengi wanashiriki:- kazi za nyumbani na huduma za kujitunza zinakuwa jukumu la pamoja, zikibadilisha maisha ya familia na kuweka mfano mpya kwa vizazi vijavyo.
· Watoa huduma wanapata haki: kupitia sheria mpya na utetezi, mamilioni wanapata malipo sawa, manufaa na mazingira salama – kutambuliwa kwa muda mrefu.
Mwelekeo huu ni halisi. Kote Afrika Mashariki na Kusini, huduma za kujitunza zimebadilika kutoka “kazi za wanawake” kuwa miundombinu ya pamoja inayowawezesha familia, jamii na uchumi. Na wakati wanawake wengi kama Marie Louise, Khadija na Noluthando wanapopata tena muda wao, kanda hii inaelekea kwenye mustakabali ambapo huduma za kujitunza zinathaminiwa na kushirikiwa, na kila mtu anafaidika.