Rais Samia Suluhu Hassan ameidhinisha kuwa Oktoba 29, 2025 ni siku ya mapumziko kutoa nafasi kwa wananchi wenye sifa stahiki wakiwemo watumishi wa umma na wafanyakazi katika sekta binafsi, kutumia haki yao ya kikatiba kupiga kura.

Taarifa kwa umma iliyosainiwa na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Moses Kusiluka imesema kuwa, uamuzi huo ni kufuatia kalenda ya Tume Huru ya taifa ya Uchaguzi (INEC) kutangaza kuwa Oktoba 29, 2025 ni siku ya kupiga kura kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu wa Rais, wabunge na madiwani.

✍ @claud_jm
#AzamTVUpdates

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *