#HABARI: Moto mkubwa umeteketeza vitu kadhaa katika moja ya majengo ya nyumba za maendeleo eneo la Mtemani wilayani Wete huko Pemba, kabla ya kudhibitiwa na kikosi cha Zimamoto na Uokozi kwa ushirikiano wa wananchi wa eneo hilo.
Sheha wa shehia ya Mtemani Mrisho Haji, ameeleza kusikitishwa na tukio hilo la moto lililotokea katika lake, na kupongeza juhudi za wananchi na kikosi cha Zimamoto katika kufanikisha kuuzima moto huo.
Kamishna wa Kikosi cha Zimamoto na Uokozi Pemba Salama Pandu Makame, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo, na kueleza kuwa kikosi chake kilifika kwa haraka na kufanikiwa kuuzima moto kabla haujasambaa katika majengo mengine.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
–
📱Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 📱kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.