#HABARI: Soko la Bidhaa Tanzania (TMX) limefanikiwa kuuza jumla ya tani 26,254 za Korosho ghafi zinazozalishwa na wakulima wanaounganishwa kupitia Chama Kikuu cha Ushirika cha TANECU Ltd, katika mnada wa kwanza wa zao la Korosho uliofanyika mkoani Mtwara.
Katika mnada huo, Korosho ziliuzwa kwa bei ya juu ya Shilingi 3,520 na bei ya chini ya Shilingi 2,550 kwa kilo, kupitia mfumo wa Kidijitali wa TMX unaolenga kuongeza uwazi, ushindani, na tija kwa wakulima nchini.
Taarifa kutoka TMX zinaeleza kuwa Korosho hizo zilihusisha jumla ya mafungu 105, na mzigo wote uliuzwa kwa mafanikio kupitia mfumo huo, hatua inayotajwa kuwa mwanzo mzuri wa msimu wa mauzo ya korosho wa mwaka 2025/2026.
Akizungumza baada ya mnada huo, Mwenyekiti wa TANECU Ltd, Karim Chipola, ameipongeza Serikali kwa kuanzisha mfumo wa TMX, na kubainisha kwamba mfumo huo umeleta mapinduzi makubwa katika biashara ya mazao kwa kuhakikisha wakulima wanapata bei nzuri na ushindani sokoni.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
–
📱Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 📱kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.