Rais Nataša Pirc Musar wa Slovenia ametangaza kuwa, nchi yake inaunga mkono kuanzishwa kwa taifa la Palestina.”

Bi Natasa amesema hayo katika mahojiano na Al-Jazeera Mubashara na kueleza kuwa, “Tuna msimamo thabiti katika kuunga mkono kuanzishwa kwa taifa la Palestina na suluhisho la serikali mbili,” Rais wa Slovenia Nataša Pirc Musar aliiambia Al Jazeera Mubashara kwamba, “Nilikuwa rais wa kwanza wa Umoja wa Ulaya kukosoa mauaji ya kimbari huko Gaza. Tunasimama na ubinadamu huko Gaza, na hili ndilo ambalo ulimwengu unahitaji sasa hivi.”

Rais wa Slovenia ameeleza bayana kwamba, “Mauaji na mauaji ya halaiki ambayo yametokea Gaza hayakubaliki. Tunaamini katika haki za binadamu na tunahitaji wanasiasa zaidi wanaoelewa mateso ya raia huko Gaza.”

Aidha amesema, jaribio la kudhoofisha Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC) (ambayo imetoa hati ya kukamatwa Benjamin Netanyahu kwa tuhuma za uhalifu dhidi ya ubinadamu) kutasambaratuisha sheria za kimataifa. Israel inazuia misaada kuingia Gaza kwa kisingizio cha uongo.”

Katika kile kinachoonekana kama hatua kubwa ya ususiaji wa kimataifa unaoendelea kufanywa dhidi ya utawala wa kizayuni wa Israel, mwezi Agosti mwaka huu (2025) Slovenia ilikuwa nchi ya kwanza mwanachama wa Umoja wa Ulaya (EU) kupiga marufuku rasmi uagizaji, usafirishaji nje, na upitishaji wa silaha na zana za kijeshi kwenda na kutoka Israel.

Hayo yanajiri katika hali ambayo, Septemba mwaka huu (2025) Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa (UNGA) lilipasisha kwa wingi mkubwa sana wa kura “Azimio la New York” linalotoa mwongozo wa kuchukuliwa “hatua zinazoonekana, katika muda maalumu na zisizoweza kutenduliwa” kuelekea kwenye uundwaji wa Dola la Palestina.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *