Mkutano wa kilele wa mabadiliko ya tabianchi unaendelea kwa siku yake ya pili hii leo katika mji wa Belem, nchini Brazil, wakati ambapo washiriki wapatao 50,000 kutoka mataifa zaidi ya 190 wanashiriki mkutano huo.

Katika hotuba ya ufunguzi, Rais wa Brazil Luiz Inacio Lula da Silva amesema mabadiliko ya tabianchi si tishio tena kwa siku zijazo na kwamba ni tishio la sasa.

 “Mabadiliko ya hali ya hewa si tishio tena kwa kizazi kijacho. Ni janga la wakati huu. Kimbunga Melisa kilichopiga eneo la Karibea na kimbunga kilichopiga kusini mwa jimbo la Brazil vimeacha athari kubwa na watu kufariki. Ukame, moto barani Afrika na Ulaya na mafuriko huko Amerika Kusini na Kusini Mashariki mwa Asia, ongezeko la hali ya joto duniani yanaeneza maumivu na uharibifu hasa miongoni mwa watu walio katika mazingira magumu zaidi” amesema Lula.

Hii leo sehemu kubwa ya mkutano huo inatarajiwa kutawaliwa na magavana wa kutoka kwenye majimbo ya  Marekani ya California na New Mexico.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *