Mshambuliaji huyo alijaribu kuingia kwenye jengo hilo la mahakama kwa miguu, lakini alililipua bomu hilo nje ya jengo, karibu kabisa na gari la polisi baada ya kusubiri kwa dakika 10 hadi 15, Naqvi aliwaambia waandishi wa habari.

“Tunachunguza kisa hicho kutokea kila upande. Hili si tu shambulizi la kawaida la bomu. Limetokea hapa Islamabad Yoyote anayehusika, awe wa humu ndani ama taifa jingine atashughulikiwa,” Waziri huyo alisema.

Pakistan Islamabad 2025 | Waziri wa Mambo ya Ndani Mohsin Naqvi akitembelea eneo kulipotokea shambulizi la kujitoa muhanga
Waziri wa Mambo ya Ndani wa Pakistan Mohsin Naqvi alipotembelea eneo kulipotokea shambulizi la bomu la kujitoa muhanga, Islamabad November 11, 2025Picha: Farooq Naeem/AFP/Getty Images

Picha zilizoonekana mitandaoni, zilionyesha watu wakiwa chini karibu na gari hilo la polisi lililolipukiwa na bomu huku wakiwa na majeraha na damu nyingi.

Katika kisa kingine, mshambuliaji wa kujitoa muhanga aliwaua watu watatu baada ya kufyatua bomu lililotegwa kwenye gari lake lililokuwa kwenye lango la kuingilia shule ya kijeshi. Kisa hicho kilitokea siku ya Jumatatu jioni katika wilaya ya Waziristan, iliyoko kaskazinimagharibi, karibu na mpaka wa Afghanistan, aliongeza waziri Naqvi.

Wanamgambo walioshambulia hatimaye waliingia shuleni humo. Na siku ya Jumanne mchana, wanamgambo watatu walikuwa bado ndani ya shule hiyo ambako kuna zaidi ya wanafunzi 500 pamoja na wafanyakazi wa shule, wamesema maafisa wa ulinzi. Hadi sasa hakuna kundi lililokiri kufanya mashambulizi hayo mawili.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *