Msimu wa Carnival huanza rasmi tarehe 11.11 majira ya saa tano za asubuhi. Na siku ya Jumanne, mapema kabisa wahudhuriaji wa mwanzo waliokuwa wamevalia mavazi ambayo mengi hustaajabisha tayari walikuwa wamekusanyika kwenye mji wa Cologne ulioko katika Jimbo la North Rhine Westphalia, magharibi mwa Ujerumani.
Ilipofika majira ya saa mbili za asubuhi, tayari kulikuwa na mistari mirefu mbele ya baadhi ya bar na maeneo ya kujivinjari. Na kama mshereheshaji mmoja wa runinga Guido Cantz alivoywahi kusema “Sio kila kitu kinawezekana mjini Cologne lakini, tunajua namna ya kujivinjari.”
Usalama waimarishwa
Zaidi ya maafisa wa polisi 1,000 na wengine 450 wa kulinda usalama wa umma na walinzi wa makampuni binafsi 1,200 wako macho kuhakikisha usalama wa wahudhuriaji kwenye sherehe hiyo ya Carnival, ambako huwa kunafurika watu katika msimu huo.
Lakini huenda wakazuia watu kuwa na visu wakati wa sherehe na kuwarai watu kujizuia kuvaa ama kuwa na vitu vinavyoweza kutumika kama silaha.
Kama ilivyokuwa mwaka uliopita, sinagogi kubwa kabisa mjini Cologne lililoko karibu na mtaa wa wanafunzi pia utalindwa kwa namna ya kipekee kabisa.
huanza tarehe 11.11 kila mwaka, ikiwa ni siku ya 11 ya mwezi wa 11. Cologne huwa ni kitovu cha sherehe hizo, lakini miji mingine ya karibu kama Dusseldorf na Bonn pia hufurika watu kuadhimisha.
Sherehe hizo humalizika siku ya Jumatano ya Majivu, ambayo huangukia Februari 18, ikiwa ndio siku ya kwanza ya kuanza msimu wa Kwaresma kwa Wakristo ulimwenguni.