Hamdi, mchambuzi wa masuala ya siasa za kilimwengu anayeishi London, alitiwa nguvuni kwenye uwanja wa ndege wa San Francisco jijini California mnamo Oktoba 26, akiwa kwenye ziara iliyoandaliwa na Baraza la Mahusiano ya Waislamu nchini Marekani, CAIR.

Mawakili wake wanadai kuwa kukamatwa kwake kulitokana na uungaji mkono wake wa Wapalestina na ukosoaji wake dhidi ya sera za Israel.

Mamlaka nchini Marekani zilidai kushikiliwa kwa mwandishi huyo kulitokana na kuzidisha muda wa kibali chake cha kuingia nchini humo, lakini wanasheria wake wanasema kibali chake kilifutwa kinyume cha sheria.

Kuachiliwa kwake kunakuja baada ya wanasheria wake kufunguwa shitaka la dharura wakiitaka serikali kuthibitisha uhalali wa kumshikilia mahakamani. 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *