Afisa wa ngazi za juu wa serikali ya Syria amesema kwamba nchi yake imejiunga kwenye muungano huo kama mwanachama wa 90, ambapo itashirikiana na Marekani kuyaangamiza mabaki ya ISIS na kuzuwia usafirishaji wa wapiganaji wa kigeni.

Rais Ahmed al-Sharaa wa Syria, ambaye mwenyewe aliwahi kuwekwa kwenye orodha ya magaidi wanaosakwa na Marekani, alikutana na Rais Donald Trump wa Marekani hapo jana mjini Washington.

Kwa mujibu wa vyanzo ndani ya ujumbe wa Sharaa, sasa Syria itaruhusiwa kurejesha mahusiano yake ya kibalozi na Washington ili kuendeleza mapambano dhidi ya ugaidi, na uratibu wa masuala ya ulinzi na uchumi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *