
Shirika la Misaada la Umoja wa Mataifa nchini Libya (UNSMIL) limezindua jukwaa la kidijitali kwa vijana wa Libya, kwa shabaha ya kuimarisha ushiriki wao katika mchakato wa mazungumzo ya kisiasa uliopangwa kufanyika nchini humo siku zijazo.
Jukwaa hilo, lililotangazwa na UNSMIL kwenye ukurasa wake rasmi wa Facebook, linawalenga wanawake na wanaume vijana wenye umri wa kati ya miaka 18 hadi 35 wanaoishi Libya, na lengo lake ni kuwapa nafasi ya kutoa maoni na mitazamo yao kuhusu masuala muhimu yaliyojadiliwa katika mazungumzo hayo. Hiyo ni sehemu ya kuunga mkono juhudi za vijana kushiriki moja kwa moja katika mchakato wa kisiasa nchini Libya.
Waliojisajili kwenye jukwaa hilo watapata fursa ya kuwatumia mitazamo yao wanachama wengine wa mazungumzo ambayo yatakuwa yanapangiwa mada maalumu, kuhakikisha kwamba sauti za vijana kutoka kote nchini Libya zinasikika na kuzingatiwa katika kufanya maamuzi ya kisiasa ya kitaifa.
“Vijana nchini Libya si tu ndio mustakabali wa nchi hiyo, bali pia ni nguzo muhimu ya mustakbali wa hivi sasa. Wao ndio walioathiriwa zaidi na mgogoro wa kisiasa wa hivi sasa na pia ndio wanufaika wakubwa wa kipindi cha mpito cha amani. Vijana wa Libya watapata fursa ya kushirikisha maoni yao na kuwa na uwezo wa kuchagua viongozi wanaowapenda,” Hayo yamesemwa na Hanna Tetteh, mwakilishi maalumu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Libya.