
Ethiopia imeishinda Nigeria na hivyo kutangazwa kuwa nchi mwenyeji wa mkutano wa Umoja wa Mataifa wa mabadiliko ya Tabianchi uliopangwa kufanyika mwaka 2027.
Nchi hiyo ya Afrika mashariki pia ilikuwa mwenyeji wa mkutano wa mwaka huu wa mabadiliko ya tabianchi barani Afrika uliofanyika mwezi Septemba.
Mkutano huo kwa jina la “Africa COP”, unatarajiwa kuchunguza nafasi ya Afrika katika kuendeleza haki na kuzipatia ufumbuzi athari za mabadiliko ya tabianchi.
Nchi za Kiafrika, ambazo zimeathiriwa kwa kiasi kikubwa na mabadiliko ya hali ya hewa licha ya nchi hizo kuwa na kiwango cha chini ya usambazaji wa gesi chafuzi, kwa muda mrefu zimekuwa zikizitaka nchi zilizoendelea duniani zigharamike pakubwa kwa ajili ya kukabiliana na hali hiyo.
Mkutano wa mwaka huu wa mabadiliko ya tabianchi-COP30 umeanza shughuli zake juzi huko Belem Brazil kwa kuwatolea wito viongozi duniani na washiriki wa mkutano huo kukabiliana na ongezeko la joto duniani.
Mkutano wa mabadiliko ya tabianchi unaofanyika Brazil utaangazia pia suala la kupunguza hewa chafu.
Nchi Mwenyeji wa mkutano ujao wa hali ya hewa wa Umoja wa Mataifa bado hajaitainishwa huku Australia na Uturuki zikiendelea kuwania nafasi hiyo.