
Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na waasi wa M23 wanaoungwa mkono na Rwanda, wametia saini makubaliano mapya ya namna ya kumaliza vita Mashariki mwa nchi hiyo.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Makubaliano hayo yametiwa saini siku ya Jumamosi na wawakilishi wa serikali na waasi wa M23/AFC chini ya msuluhishi wa mgogoro huo, taifa la Qatar jijini Doha.
Hatua hii inakuja, baada ya DRC na M23 kutia saini maelewano mengine ya namna ya kusitisha vita mwezi Julai, lakini vita vimeendelea kushuhudiwa huku kila upande ukimlaumu mwenzake kwa kukiuka kilichokubaliwa.
Utiaji saini huu mpya,pia umeshuhudiwa na wawakilishi kutoka Marekani, huku msuluhishi mkuu Mohammed Al-Khulaifi, akisema pande hizo mbili zimekubaliana kuendeleza jitihada za kupata amani ya kudumu.
Aidha, Al-Khulaifi amesema Qatar itaendelea na jitihada za usuluhishi kuhakikisha kuwa pande zote mbili zinakubaliana na kutia saini mkataba wa kudumu.
Haya yanajiri wakati waasi wa M 23/AFC wakiendelea kudhibiti miji na Bukavu na Goma tangu mwezi Januari mwaka huu, katika mzozo ambao umesababisha maelfu kupoteza maisha.